WANANCHI KATA YA KATUMBA WILAYANI MPANDA WAITAKA SERIKALI KUTOA UAMUZI KUHUSU NAFASI YA UDIWANI ILIYOACHAWA WAZI



Baadhi ya wakazi wa Kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo mokoani Katavi  wameitaka serikali kutoa tamko kuhusu hatima ya nafasi ya Udiwani katika Kata hiyo kufuatia Diwani aliyekuwepo kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela


Wakizungumza na Mpanda radio fm kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa nafasi ya Diwani kama msimamizi mkuu wa shughuri za  maendeleo haipaswi kuwa wazi bila ufafanuzi wowote.

Mpanda radio fm imemtafuta Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Raphael Karinga ili atoleee ufafanuzi ikiwemo hatua walizo zichukua ambapo amedai kukabiliwa na majukumu na kwamba atazungumza mara baada ya kuhitimisha majuku hayo.

Diwani wa kata hiyo Seneta Baraka amefungwa tangu mwaka jana akidaiwa kupokea hongo kwa mfugaji mmoja ili amuidhinishe kufanya shughuri za ufugaji katika eneo lililo zuiliwa na Mahakama.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.