Wanafunzi watano wakamatwa kwa kupata mimba

Jumla ya wanafunzi watano wa kike wa shule za sekondari Tandahimba waliopata mimba mwaka 2017 wamekamatwa pamoja na wazazi watano baada ya kufanyika msako. 
Katibu Tawala wa wilaya ya Tandahimba, Mohamed Azizi amesema hayo leo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Sebastian Waryuba baada ya kufanikiwa kuwakamata wanafunzi hao wakiwa na watoto wao huku wahusika waliosababisha kukatiza masomo yao kutokomea kusikojulikana. 
“Tumefanikiwa kuwakamata wazazi na wanafunzi watano wakiwa wamejifungua kati yao mmoja ameacha shule akiwa kidato cha nne, huku mwingine akiwa kidato cha tatu na cha pili baada ya kuzungumza nao wote wamesema hakuna hata mmoja ambaye anapata huduma kutoka kwa wahusika ambao wamewapa mimba hali ambayo inawapa shida wazazi wao kuwahudumia,” amesema Azizi 
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkolea, Selemani Abduli amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa mkuu wa shule hatua ambazo amezichukua ni kuwakamata wahusika wote wawili na kuwapeleka katika kituo cha polisi.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.