Walio potea wakienda kutafuta uyoga wapatikana
Watoto wa nne pamoja
na mama mmoja waliopotea tangu 8/1/2018
walipokuwa wameenda kuokota uyoga porini katika
kijiji cha Kambuzi A kata ya Katumba katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo
Mkoa wa Katavi wamepatikana.
Akizungumza na Mpanda redio Mwenyekiti wa kijiji cha Kambuzi
A Bw Naftali Stephano Amesema amepokea taarifa kutoka kwa mchana mbao mmoja
ambaealiwahifadhi watu hao kambini kwake kwa muda baada ya watu hao kusema
wamepotea
Mmoja wa wazazi ambao walipotelewa na watoto hao amesema
amepokea taarifa za kupatikana kwa watoto hao na mama mmoja na tayali wanafanya
utalatibu wa kuwa fuata huko polini
Kumekuwepo na tabia ya wazazi katika maeneo mbalimbali hapa
nchini hususani vijiji nyakati za masika kuwa tuma watoto porini kwenda kuokota
uyoga hali ambayo hupelekea miongoni mwao kupotea porini

Comments
Post a Comment