Wakulima wa zao la Tumbaku wa Chama Cha Msingi Cha Ukonongo katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamelalamikia kucheleweshewa malipo
Katavi:
Wakulima wa zao la Tumbaku wa Chama Cha Msingi Cha Ukonongo katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi wamelalamikia kucheleweshewa malipo ya zao la tumbaku katika msimu wa
mwaka uliopita.
Wakizungumza na Mpanda redio kwa nyakati
tofauti wamesema licha ya
mchanganuo wa malipo kufanyika bado wakulima wengi hawajapatiwa fedha zao hali
ambayoinasababisha ugumu wamaisha katika
msimu huu wa kilimo .
Kwa upande wake
mwenyekiti wa chama hicho cha msingi Godfley Malilo amesema changamoto iliyopo
ni uingizwaji wa ushuru wa chama umecheleweshwa lakini hatua za kuanza malipo
hayo yanatarajiwa kuaanza wiki ijayo.
Chama hicho cha msingi kinawakulima wa tumbaku zaidi
ya elfu mbili na kimekuwa kikichangia kwa kiasi kikubwa katika pato la
halimshauri ya wilaya ya Mlele.
Source Paul mathius
Editor Alinanuswe Edward.

Comments
Post a Comment