WAKULIMA WA ZAO LA KOROSHO WALIOKUWA WANADAI 800 WAMELIPWA.


Deni la zaidi ya shilingi milioni 800 ambalo lilikuwa likidaiwa na wakulima wa Korosho kwa msimu wa 2016/2017 kwa vyama vya msingi (AMCOS) hatimaye limelipwa.
Mwenyekiti wa bodi ya chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara Cooperative Union (MAMCU) Joseph Kidando amesema tayari kiasi hicho cha fedha kimeingizwa katika akaunti za vyama vya msingi kwaajili ya  kugawanywa kwa wakulima.
Aidha mwenyekiti huyo amesema wamelazimika kulipa deni hilo kutokana na wao kuwa walezi wa AMCOS na wakulima kwa ujumla na ametaja sababu za kuchelewesha kulipwa kwa fedha hizo ni upotevu wa fedha uliosababishwa na makosa ya viongozi wa AMCOS.
Kwa upande mwingine Kidando ameeleza kuwa sababu nyingine kubwa iliyosababisha upotevu wa fedha hizo ni kuingizwa kimakosa katika akaunti tofauti za vyama vya msingi, ambapo baadhi ya viongozi wasiowaaminifu waliamua kuzifanyia matumizi binafsi.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.