WAKULIMA MPANDA/ KATAVI WAITAKA SERIKALI KUTENGANISHA MAENEO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA
Baadhi ya wakazi wa
kata ya Magamba Manispa ya Mpanda mkoani Katavi wameitaka serikali kutenga
maeneo ya wafugaji na wakulima ili kuepusha migogoro ya ardhi inayojitokeza
mara kwa mara
Wakizungumza na Mpanda
Radio kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema wakulima na wafugaji
wanapoendesha shughuli zao katika eneo moja huchangia mifarakano isiyo ya
lazima na kushauri wafugaji kutengewa eneo tofauti na wakulima ili kuondoa
mwingiliano
Kwa upande wake Bi Anna
Thomas ambaye ni mwenyekiti wa serikali za mitaa amekiri kuwepo kwa migogoro ya
mara kwa mara baina ya wakulima na wafugaji na kuongeza kuwa inachangangiwa na
wafugaji kuwa na mifugo mengi kwenye eneo dogo
Philemone Tesha Afisa
kilimo wa kata ya magamba amesema serikali ina mpango wa kutenga maeneo ya
kuchungia yatakayokuwa tofauti na mashamba japo hakubainisha wazi mpango huo ni
lini utaanza kutekelezwa

Comments
Post a Comment