Wahamiaji haramu 297 wameokolewa




Wahamiaji haramu 297 wameokolewa na jeshi la majini    kwenye eneo la bahari lililoko karibu na pwani ya mji wa Garrabulli, kilomita 60 mashariki mwa Tripoli.

Msemaji wa jeshi la majini la Libya Bw. Ayob Qassem, amesema na kwamba vifo vya watu wawili katika tukio hilo vimetokana na boti walizokuwa wakisafiria kujaa wahamiaji kupita kiasi.

Libya imekuwa nchi inayotumiwa na wahamiaji haramu kuvuka bahari ya Mediterranean kwenda Ulaya, kutokana na kukosekana kwa usalama nchini humo, baada ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani mwaka 2011.


SOURCE: CRI

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.