Utekelezaji wa agizo la Wizara ya Elimu kuweka kiwango sawa cha ufaulu kwa shule za binafsi na serikali, umekuwa kaa la moto.
MPANDA
Walimu wa shule za sekondari za binafsi mkoani Katavi
wameelezea kuwepo kwa changamoto utekelezaji wa agizo la kuweka
kiwango sawa cha ufaulu kwa shule za binafsi na serikali.
Kauli hiyo inakuja kutokana na maagizo ya serikali
kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ambapo shule binafsi zimetakiwa
kubadilisha mfumo kwa ufaulu wa wanafunzi na kuwa sawa na shule za serikali.
Wamesema itawalazimu kubadilika japo hatua hiyo
haitamjenga mwanafunzi kitaaluma kwani wengi wao wanaosomea katika shule
binafsi ni wale walioshindwa kufaulu kwenye shule za serikali.
Hatua hiyo ya wizara ya elimu imetajwa kuwa ni moja
ya kupunguza upatikanaji wa wanafunzi watakao jiunga na shule binafsi kwani
kutakuwa hakuna umuhimu kutokana na usawa katika viwango vya ufaulu.
Source Esther Baraka
Editor Aliananuswe
Edward

Comments
Post a Comment