Sugu apelekwa gerezani
Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi leo Januari 16, 2018 amepelekwa gereza la Rwanda jijini Mbeya baada ya kukosa dhamana kufuatia kesi inayomkabli ya kutoa maneno ya uchochezi katika moja ya mkutano wake mwaka jana.

RPC wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Mbunge huyo leo alipelekwa mahakamani kwa kosa hilo na mahakama imemnyima dhamana na kupelekwa katika gereza la Rwanda.
"Leo tulimpeleka mahakamani kutokana na Mkutano wake wa hadhara ambao aliufanya tarehe 31 Disemba mwaka jana kuna maneno ambayo alitamka hayakuwa mazuri kwenye ule mkutano pamoja na kwamba katika maombi yake kwenye huo mkutano alisema anataka anataka kuzungumzia maendeleo pamoja na kuwatakia kheri ya mwaka mpya 2018 lakini matokeo yake alizungumza mambo mengine ambayo yanaweza kujenga chuki kati ya wananchi na serikali kwa hiyo tulipeleka jarada kwa wanasheria wa Serikali ikaonekana kuna makosa ya kujibu mahakamani kwa mujibu wa sheria"
Aidha RPC huyo aliendelea kusema kuwa baada ya kupelekwa mahakamani Mbunge huyo amenyimwa dhamana na kupelekwa magereza.
Comments
Post a Comment