SHEINI AELEZEA UKUAJI WA UCHUMI MIAKA 54 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili kuwa chachu ya kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa uwekezaji miradi mikubwa ya maendeleo visiwani humo.

Amesema hayo Katika maadhimisho  ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyo udhuriwa na Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na viongozi wengine wa serikali ambapo  ameelezea kukua kwa kasi ya uchumi katika visiwa hivyo na kuwa lengo la kuimarisha uchumi ni endelevu.

Ameutaja mradi wa kusaidia kaya masikini  Tasaf namba tatu  kuzinufaisha kaya zaidi ya 32478 ikiwa nikiwango kikubwa zaidi.

Aidha amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwainua wakulima kwa kusimamia misingi ya kisera akilitaja zao la kalafuu Kama zao lenye tija zaidi.


Zanzimbar iliungana na Tanganyika mnamo apr 26, 1964 chini ya  waasisi hayati Sheihk Abeid Aman Karume na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.