Serikali ya Ethiopia imewakamata watu 107 kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizotokea hivi karibuni katika eneo la mpaka wa mikoa ya Somali na Oromia.
ADDIS ABABA
Serikali ya Ethiopia imewakamata watu 107 kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizotokea hivi karibuni katika eneo la mpaka wa mikoa ya Somali na Oromia.
Kamishna wa tume ya polisi ya Ethiopia Abiyu Assefa amesema watuhumiwa 98 kati ya hao waliokamatwa wanatokea mkoa wa Oromia na wengine tisa kutoka mkoa wa Somali.
Mapigano makali katika eneo la mpaka wa mikoa hiyo miwili yaliyotokea mwezi Septemba mwaka jana yalisababisha mapigano ya kikabila yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa.
Mbali na vifo hivyo vinavyotajwa kutokea halikadhalika mamia ya watu walikimbia makazi yao wakihofia kuuwawa.

Comments
Post a Comment