Raisi wa Rwanda Paul Kagame amewasili nchini kwa ziara ya siku moja.
DAR ES SALAAM
Raisi wa Rwanda Paul Kagame amewasili nchini
kwa ziara ya siku moja.
Paul Kagame amepokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ambapo atakuwepo nchini kwa
ziara ya siku moja ikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano mzuri kati ya kati ya nchi hizo mbili.
Serikali ya Rwadwa ina
mpango wa kuboresha elimu na huduma za afya ili kufikia lengo la utoaji huduma
kwa kiwango cha juu na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.
Aidha Raisi wa Tanzania John Magufuli na mgeni
wake Paul kagame wa Rwanda baada ya kupokelewa
uwanja wa ndege Mwalimu Julius Nyerere
wameelekea ikulu jijini Dar es salam kwa mazungumzo zaidi.

Comments
Post a Comment