Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Rais wa Rwanda Paul Kagame waahidi Neema ya Kiuchumi kwa wananchi wa nchi zao.
Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi ya Rwanda ili kuchechea maendeleo.
Amesema hayo Ikulu jijini Dar es Salam alipokuwa akizungumza mara baada ya kumpokea rais wa Rwanda Paul Kagame na kufanya mazungumzo yaliyojikita zaidi katika fulsa za kiuchumi na ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.
Rais Magufuli pia amezungumzia ujenzi wa reli ya standard geji kutoka Isaka mpaka Kigali Rwanda kuwa ipo tayari katika hatua ya upembuzi wa awali ambayo inatajwa kuwa kichocheo cha uchumi.
Kwa upande wa Rais Kagame amesema katika masaa machache waliyo kaa Ikulu na kuzungumza na Mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli yame jenga mstakabari wa pamoja kiushirikiano katika Nyanja mbali mbali za kimaendeleo.
Paul Kagame ambaye anatalaji kugombea kuwa mwenyekiti wa umoja wa afrika AU ameeleza kuwa atafanya juu chini kuhakikisha vijana wa kiafrika hawazikimbii nchi zao kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika.

Comments
Post a Comment