Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Mhe.Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.
John Pombe Magufuli leo amemteua Mhe.Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa
Madini.
Mhe.Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na alikuwa
Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.
Kufuatia uteuzi huo,Wizara ya Madini sasa itakuwa na
Waziri na Naibu Mawaziri wawili.
Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya rais Ikulu Gerson Msigwa amesema, rais Magufuli amefanya
uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika
Wizara ya Madini.
Mhe.Doto Mashaka Biteko anatarajiwa kuapishwa
Jumatatu Januari 08 Januari mwaka huu Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Comments
Post a Comment