Rais Magufuli apiga marufuku wanafunzi kufukuzwa shule kwa kutotoa michango


Rais John Magufuli amepiga marufuku shule za msingi na sekondari nchini kuwafukuza wanafunzi kwa sababu ya kutochanga michango mbalimbali ya shule.
Akizungumza leo Jumatano Januari 17, 2018 Ikulu Dar es Salaam baada ya kukutana na mawaziri wanaohusika na sekta hiyo amesema ikitokea katika wilaya mwanafunzi akarejeshwa nyumbani kwa kushindwa kulipa michango, mkurugenzi wa wilaya atafukuzwa kazi.
“Kwa taarifa hii mkawaeleze wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi. Nikisikia kuna shule katika wilaya fulani ambayo watoto wanarudishwa kwa sababu hawajachangia kitu fulani, huyo mkurugenzi ajihesabu hana kazi,” amesema Rais Magufuli na kuongeza,
“Hii waanze kutekeleza kuanzia leo. Maofisa elimu wote wakasimamie hili, haiwezekani tukawa tunatoa elimu bure halafu tutengeneze kero kwa watoto wanaosoma.”



Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.