Nusura ndege yenye abiria 168 itumbukie baharini Uturuki
Hofu iliwakumba abiria wakati ndege waliyokuwa wakisafiria ilipopoteza mwelekeo kwenye uwanja wa ndege huko Uturuki na kukimbia kwenda mteremko ulio kando ya bahari.
Ndege hiyo ya shirika la Pegasus Boeing 737-800 iliyokuwa na abiria 168, ilikuwa imetoka mjini Ankara na ilitua uwanja wa Trabzon kwenye Black Sea siku ya Jumamosi.Kila mtu aliyekuwa ndani ya ndege hiyo aliondolewa salama, kwa mujibu wa gavana wa mkoa Yucel Yavuz.

Comments
Post a Comment