Nchi za Afrika masharki za tajwa katika ukiukwaji wa haki za binadamu


Ripoti ya Shirika la kutetea haki za binaadam Human Right Watch ya mwaka 2018 imeangazia haki za binaadamu namna zilivyokiukwa katika mataifa kadhaa barani Afrika.

 Ikianza na Tanzania, ripoti hiyo inasema baada ya kuingia serikali awamu ya tano ilidhamiria kuondoa tatizo la rushwa serikalini na kuongeza uwajibikaji kwa manufaa ya wananchi wa kawaida, lakini badala yake uhuru wa kukosoa umekandamizwa ikiwemo kufungwa kwa vyombo vya habari.

 Aidha imeeleza kuwa watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati wa asasi za kiraia na maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa wamekumbana na aina mbalimbali za vitisho na kuwekwa vizuizini bila sababu za msingi kunakofanywa na mamlaka za serikali.

 Nchini Kenya nako Shirika hilo limebaini kuwa mauaji yaliyofanywa na polisi katika mitaa ya mabanda hayakuchunguzwa hadi  leo. 

Aidha katika kipindi cha kabla na baada ya uchaguzi shirika hilo limesema polisi na vikosi vingine vya usalama vimetumia nguvu kupita kiasi kuwakabili waandamanaji hasa katika ngome za upinzani.
Source DW
Editor Alinanuswe EDWARD

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.