NAPE ASHITUSHWA NA MWINGILIANO WA SHUGHURI ZA KISERIKALI NA CHAMA

Nape Nnauye amesema kuwa kuna wakati inakuwa ni vigumu sana kumtofautisha Rais wa nchi na Mwenyekiti wa CCM kwa kuwa mtu huyo anakuwa ni mmoja na kwenda mbali zaidi kuwa kuna wakati huwa kuna kuwa na mvutano kati ya wanachama na viongozi wa ulinzi na usalama katika baadhi ya matukio ambayo Rais anahudhuria.
"Bahati mbaya ni ngumu sana kumtofatisha Magufuli Rais wa Tanzania na Magufuli Mwenyekiti wa CCM kwa kuwa huyu mtu ni mmoja kwamba yeye ndiye mwenye vyeo vyote viwili lakini ni rahisi kuzitofautisha shughuli kwamba anapofanya mambo ambayo yanaihusu taasisi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusichanganywe na shughuli za CCM inawezekana ikafanyika hivyo" alisema Nape Nnauye
Aidha Nape Nnauye aliendelea kusema kuwa "Niliona katika mkutano mmoja nadhani ni Arusha pale ilikuwa ni paredi ya wanajeshi nadhani halafu baadaye nikaona shughuli za chama zimeingia, ukiangalia hapa unapata ukakasi fulani na kusema nadhani hili lina tabu ndiyo maana nasema wapi tuchore mstari wakati mwingine ndiyo inakuwa ngumu hivyo muda mwingine si suala la upendeleo bali ni wapi tuchore mstari tutofautishe shughuli za kiserikali na shughuli za chama"

Comments
Post a Comment