Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amemfungia msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind kujihusisha na sanaa kwa muda wa miezi sita
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amemfungia msanii
Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind kujihusisha na sanaa kwa muda wa miezi
sita.
Akizungumza
leo Jumapili Januari 7 jijini Dar es Salaam, Shonza amesema amechukua hatua
hiyo kutokana na msanii huyo kutoa wimbo uitwao ‘viduduwasha’ usio na maadili.
Msanii
huyo pia amekutwa na kosa la kufanya kazi ya sanaa bila kusajiliwa na
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuweka mtandaoni picha ya nusu utupu kinyume
na maadili.
‘’Kumekuwa
na wimbi kubwa la wasanii kutoa nyimbo zenye maneno ya matusi na zisizo na
maadili, pamoja wanawake kupiga picha wakiwa wamevaa nusu utupu na kuweka picha
hizo katika mitandao,” amesema Shonza na kuongeza,
“Nataka
kuwapa angalizo wasanii wenye tabia hizi kuwa Serikali inawafuatilia kwa karibu
na mwaka huu tumeanza na huyu na wengine wanafuata kama msanii Gift Stanford
maarufu kama Gigy Money na Jane Rimoy maarufu kama Sanchi.”
Shonza
amemtaka msanii Gigy Money kufika ofisini kwake haraka, kwa maelezo kuwa
alimtaka afanye hivyo siku za hivi karibuni lakini ameshindwa kuitikia wito
wake.
Katibu
Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amesema kwa mujibu wa kanuni
31 (1) ya baraza ya mwaka 2005, inaeleza msanii kufanya kazi bila
kusajiliwa ni kosa na anaweza kufungiwa, pia kwa upande wa mavazi zinasema
msanii anatakiwa kuvaa mavazi yenye staha yasiyomdhalilisha wala
kudhalilisha watazamaji wake.
“Napenda
kuwasisitiwa wasanii wote ambao wanajijua kuwa hawajasajiliwa Basata kuja
kujisajili haraka na kwa wale waandaji wa kazi za sanaa kama waongozaji,
waandaaji na wamiliki wa studio za kurekodi kazi za
sanaa ambao hawajasajiliwa nao waje kujisajili haraka,” amesema.

Comments
Post a Comment