Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile ameitaka jamii kuheshimu na kulinda haki za watoto


KATAVI:

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amewataka watanzania kuhakikisha watoto wote nchini wanapatiwa haki zote za msingi katika maisha yao ikiwemo haki za kuishi na kulindwa.

Dkt.Ndugulile ametoa wito huo mapema wiki hii Mjini Mpanda wakati akizungumza na Makundi mbalimbali ya wananchi ambayo yamepewa jukumu la kuelimisha jamii kuhusu haki za mtoto na kuwaibua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Aidha DK.Ndugulile amesema serikali itaendelea kushirikiana na Shirika la JSI la Marekani linalojihusisha na masuala ya jamii ikiwemo kudhibiti mambo yanayomkatisha mtoto kutimiza ndoto zake hasa kielimu.
Jumla ya watoto 1200 na wazazi walezi 506 waishio katika mazingira hatarishi wameibuliwa na kupatiwa huduma katika maeneo mablimbali ya Manispaa ya Mpanda.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.