Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi aelezea mafanikio




TANGANYIKA:
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando amesema watakaokiuka zoezi la kutambua na kuweka alama ya chapa katika mifugo atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria na taratibu za nchi.

Muhando ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaaji wa ilani ya chama cha Mpainduzi CCM katika kipindi cha mwezi Julai mpaka Desemba 2017 kupitia kikao maalumu cha chama hicho ambacho kimefanyika Mjini Mpanda.

Aidha amesema,mpaka kufikia Desemba mwaka jana,zaidi ya ng’ombe laki moja na elfu hamsini wametambuliwa na kuwekewa alama ya utambuzi katika vijiji hamsini ambapo zoezi hilo bado linaendelea katika vijiji vinne vilivyosalia Wilayani humo.

Kwa upande wa wajumbe wa kikao hicho,wamesema utekelezwaji wa agizo hilo la seriikali kufanyika nchi nzima litapunguza uharibifu wa mazingira,kutokomeza wizi wa mifugo na kutatua migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.
Source Issack Gerlad

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.