Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Salehe Mhando aeleza siri ya ukuaji wa kiuchumi na maendeleo katika Wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya  ya Tanganyika Salehe Mhando (katikati) akikagua Mwalo wa Kisasa wa Kata ya Ikola katika Mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika iliyopo mkoani Katavi Salehe Mhando,amesema miradi mingi ya maendeleo Katika wilaya hiyo imekuwa ikitekelezwa kwa wakati ili kuendana na kasi ya serikali awamu ya tano.

Mwandishi wa habari Alinanuswe Edward wa Mpanda radio fm akipiga picha mara baada ya kufanya mahojiano na maafisa uvuvi katika mwalo huo.

Miongoni mwa miradi iliyotekelezwa ni pamoja na mradi mkubwa wa maji uliopo kijiji cha Majalila unao endeshwa na nguvu ya Umeme wa jua, ujenzi wa hostel Katika Shule ya Sekondari Kabungu, ambao umefiki hatua ya mwisho, ukarabati wa Mwalo wa Kisasa Katika mwambao wa ziwa Tanganyika maarufu Kama mwalo wa Ikola, unaotumika kuongeza thamani ya Mazao ya Samaki ili kuongeza tija kwa wa vuvi.

Wilaya ya Tanganyika ni wilaya mpya yenye umri wa mwaka mmoja na mwezi kadhaa ambapo wakazi wa eneo hilo hujishughulisha na Kilimo, Uvuvi, ufugaji na utengenezaji wa thamani zitokanazo na utajiri wa misitu uliobebwa na uoto wa asili.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando akikagua ujenzi wa jengo la Utawala la halmashauri linalojengwa katika kijiji cha Majalila

Salehe Mhando anasema haoni fahari kuwa mkuu wa wila pekee bali faraja yake kubwa ni kuona shabaha yake ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi Katika wilaya hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.