Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amepiga marufuku vitendo vya wanaume walio kwenye ndoa kupiga wake zao, akisema atakayebainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

IRINGA.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amepiga marufuku vitendo vya wanaume walio kwenye ndoa kupiga wake zao, akisema atakayebainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari Tagamenda wilayani Iringa ambapo amefafanua kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na baadhi ya familia kuchukulia vitendo hivyo kuwa ni vya kawaida.
Ameeleza kuwa hadi sasa ameshawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wanaume watatu na kuwataka wanawake wanaopatwa na masaibu hayo kutoa taarifa kwake ili achukue hatua badala ya kuona kuwa vitendo hivyo ni sehemu ya maisha yao.
Aidha amebainisha kuwa hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana katika familia endapo mama na baba wanaingia katika ugomvi na hata kuumizana.

Hatua ya Kasesela kuwataka wanawake kutoa taarifa kwa vitendo vya ukatili ikiwemo vipigo imepokelewa  kwa furaha na wanawake waliohudhuria mkutano huo ambao wamesema itasaidia kurejesha heshima na utu.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.