MKUU WA MKOA WA TABORA AGREY MWANRI AWASAKA WAZAZI NA WALEZI AMBAO HAWAJAWAPELEKA WANAFUNZI WALIO FAULU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA
TABORA
Serikali Mkoani Tabora imeagiza kukamatwa mara moja
wazazi au walezi ambao hadi kufikia leo
Jumatatu ijayo watakuwa wameshindwa kuhakikisha kuwa watoto wao
waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza mwaka huu watakuwa hawajaripoti
katika Shule walizopangiwa.
Agizo hilo limetolewa mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kupata taarifa kutoka kwa Afisa Elimu Mkoa
iliyokuwa ikionyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na
Kidato cha kwanza mwaka 2018 bado wengi wao hawajaripoti katika Shule
walizopangiwa.
Amesema kuwa kufikia leo jumatatu anataka kupata taarifa na majina ya wanafunzi
wote waliochangiwa, na ambao hawako shuleni ikiwa na majina ya wazazi wao
ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa kwa kosa la kumkoshesha
watoto haki ya kupata elimu.
Mwanri ameongeza kuwa viongozi wa
kuanzia mitaa, vitongoji, vijiji , Kata na Wilaya ni vema wahakikishe
wanawatafuta watoto wote waliochaguliwa ambao hawako shuleni ili kujua walipo
na wanafanya nini kwa kuwa inawezekana wapo ambao tayari wameshaozeshwa

Comments
Post a Comment