MKUU WA MKOA WA NJOMBE OLE SENDEKA AKANA KULITUSI BUNGE



NA: Edward Barnaba


Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amekana kuhusika na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limemomonyoka.

Katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Longido,  amesema taarifa hiyo iliyoanza kusambaa tangu juzi inapaswa kupuuzwa.

Amezielezea tuhuma hizo kuwa Propaganda zinazofanywa na vyama vya upinzani kutokana na hofu ya mambo ya kisiasa na hivyo kumgombanisha na serikili.

Wakati Ole Sendeka akieleza hayo, Spika wa Bunge, Job Ndugai  ameiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji mkuu huyo wa mkoa kuhusu kauli anayodaiwa kuitoa.


OlesendekaSendeka ambaye amewahi kuwa   mbunge wa Simanjiro anadaiwa kutoa kauli zilizo ashiria kejeli kwa chombo hicho cha kutunga sheria ikiwa ni siku chache baada ya kusambaa kwa kipande cha sauti inayodaiwa kuwa ni yake, akieleza jinsi Bunge kutokuwa madhubuti.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.