Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka kuchunguzwa kwa kudhalilisha bunge.


DODOMA

Spika wa Bunge Job Ndugai ameiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujadili na kuchunguza kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka inayodaiwa kudhalilisha bunge.

Hatua hizo za Mh. Spika zimekuja baada ya kauli zinazodhaniwa kuwa ni za Mh. Olesendeka zikiashiria kejeli na dharau kwa Bunge ambazo zilikuwa zikitamkwa kwa Lugha ya Kimasai, kiswahili na Kingereza.

Taarifa iliyotolewa kwa wanahabari imesema kwamba , Spika ameelekeza kuwa Kamati hiyo  imuite na kumhoji Kiongozi huyo  ikiwa ni pamoja na kuchunguza ukweli na dhamira ya kauli hizo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.


Kauli zinazodaiwa kuwa ni za Ole- Sendeka zilisikika zikisema kwa  bunge limemomonyolewa. 

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.