MBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA KATAVI KUPITIA CHADEMA ASEMA KATA YA KATUMBA H/MASHAULI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUTOKUWA NA DIWANI NI UCHELEWESHAJI WA MAENDELEO.
KATAVI:
Mbunge wa viti maalumu
mkoa wa Katavi kupitia Chadema Rhoda
Kunchela amesema kitendo cha kata ya
katumba halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kutokuwa na diwani ni kuchelewesha
maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo.
Hayo yamebainishwa leo na
Mbunge huyo wakati akizungumza na Mpanda Radio na kusema kuwa wananchi wanakosa
uwakilishi na kushauri uchaguzi ufanyike
ili apatakane diwani mwingine .
Diwani aliyekuwa
akiongoza kata hiyo Mh Seneta Baraka amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela
tangu mwaka uliopita kwa kosa la kupokea
rushwa.
Katika hatua nyingine Mh
Kunchela amezungumzia ziara aliyoifanya
mwenyekiti wa Bawacha taifa Halima Mdee
amabye pia ni mbunge wa jimbo la kawe na kusema ziara hiyo imefanyika mkoani katavi ikilenga
kuimarisha uhai wa chama hicho.

Comments
Post a Comment