Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi yakili kushindwa kuandaa maadhisho ya siku ya walemavu duniani kwa miaka 2 mfululizo.
MPANDA.
Mkurugenzi
wa Manspaa ya Mpanda Michael Nzyungu amekiri kutofanyika kwa maadhimisho ya
siku ya walemavu duniani kwa mwaka uliopita kutokana na kutokuwa na mawasiliano
ya kutosha kati ya halmashauri hiyo na ofisi ya mkoa.
Akizungumza
na Mpanda Redio kwa njia ya simu Bwana Nzyungu amesema mkoa ndio wenye jukumu
la kupanga sherehe katika ngazi ya
halmashauri na wilaya jambo ambalo halikufanyika.
Katika
hatua nyingine amesema kuwa suala la
bajeti sio tatizo kiasi cha kukwamisha
maadhimisho hayo na kauhidi kuwa mwaka huu manispaa itahakikisha tatizo hilo
halijirudii tena.
Mkoa wa katavi umeshindwa kuaandaa
Maadhimisho ya siku ya walema duniani kwa miaka miwili mfululizo ambayo hufanyika decemba tatu kila mwaka.

Comments
Post a Comment