Makusanyo yamapato katika Halmashauri ya Manispaa yaongezeka kwa 78%


Makusanyo yamapato katika Halmashauri ya manispaa ya Mpanda yameongezeka nakufikia 78% tofauti na ilivyo kuwa mwezi wa kumi na moja mwaka jana ambapo walikusanya shilingi milioni 370.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mapata wa manispaa  ya Mpanda  Mola Elias Wakati akizungumza na Mpanda Redio ambapo ameeleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 480 Katika kipindi cha mwezi wa 12/ 2017 zimeweza kupatikana.
Aidha Mola amesema kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya wafanyabiashara kuwa wazito katika kutoa kodi na kuwaommba kujenga tabia ya kulipa kodi hali ambayo itasaidia kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

Kwa upande wafanyabiashara katika manispaa ya Mpanda wamesema kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi ili kuisaidia serekali kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo 

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.