Madiwani watatu wa Chadema, katika halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha , wametangaza kujiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ( CCM).



Madiwani watatu wa Chadema, katika halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha , wametangaza kujiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ( CCM).

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Longido, Jumaa Mhina alithibitisha leo  Januari 10 kujiuzulu kwa madiwani hao, Jacob Silas Mollel Kata ya Elang'atadapash, Elias Mepukori Mbao  Kata ya Kamwaga na  Diyoo Lomayani Laizer Kata ya Olmolog.

Mhina amesema  sababu za kujiuzulu madiwani hao wamezitoa kuwa ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi, kuinua uchumi na pia kurejesha nidhamu kazini.


Amelezea  barua za madiwani ghao kwamba wanafanya  utaratibu wa  kuziwasilisha tamisemi kwa ajili ya utaratibu wa kisheria ili kuwezesha kufanyika uchaguzi mdogo baada ya Tume kupata taarifa.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.