Maandamano ya ghasia kupinga mfumuko wa bei yaendelea Tunisia
Kumekuwa na muendelezo wa siku tatu wa ghasia za maandamano nchini Tunisia katika mji mkuu wa Tunis na miji mingine ya nchi hiyo.
Polisi wamekuwa wakirusha mabomu ya machozi kwa kundi kubwa la watu ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya mfumuko wa bei ambao unaathiri upatikanaji wa mahitaji muhimu.
REUTERS
Waziri mkuu , Youssef Chahed amelaani kwa kile alichokiita kuwa ni hakikubaliki kwa kuwepo kwa fujo za waandamanaji.
Kwa upande wao waandamanaji ,nao pia wametoa malalamiko yanayofanana juu ya polisi.
REUTERS
"Maandamano ni juu ya bei kuwa ghali , wamepandisha, nadhani hii ni hali ngumu sana kubadilika , labda kama rais huyu tutamuondoa"
Comments
Post a Comment