LOWASA ASEMA ALIITWA IKULU NA KUOMBWA NA RAIS MAGUFULI ILI AJIUNGE NA CCM

Mjumbe wa kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, Edward Lowassa amefichua kuwa Rais John Magufuli alimuomba arejee chama tawala cha CCM wakati wa mazungumzo yao juma lililopita .
Katika taarifa iliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kwa waandishi wa habari Lowassa ameeleza "ujumbe wa Rasi Magufuli ulikuwa kunishawishi kutaka nirejee CCM, suala ambalo sikukubaliana nalo na nilimueleza Rais ya kwamba uamuzi wangu wa kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA haukuwa wa kubahatisha"
Wiki iliopita, kiongozi huyo wa upinzani nchini Tanzania, ambaye pia ni Waziri mkuu wa zamani, alikutana na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Ikulu na kumsifu sana kwa kazi anayoifanya.
Nukuu ya Lowassa
Ni hatua ambayo iliwashangaza wengi kwani si kawaida kwa kiongozi huyo kumsifu Rais Magufuli kwani kwa muda amekuwa akikosoa utawala wake.
Bw Lowassa aliwania urais kupitia chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 lakini akashindwa na Dkt Magufuli aliyewania kupitia Chama cha Mapinduzi.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.