Lissu aitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati upelelezi wa tukio la kushambuliwa kwake



NAIROBI

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema kuwa kesho Januari  atasafiri na kutoka nje ya Kenya kwenda kufanyiwa matibabu zaidi kufuatia shambulio la kupigwa risasi lililotokea mwaka jana. 

Amesema  hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa nje ya hospitali ya Nairobi na kusema kuwa amekuwepo hapo kwa takribani miezi minne akifanyiwa matibabu lakini sasa anakwenda kufanyiwa matibabu zaidi sehemu nyingine. 

Mbali na hilo Tundu Lissu ameendelea kusema kuwa shambulio lake la kupigwa risasi ni tukio la kisiasa ndiyo maana viongozi wa bunge wamekuwa wakishikwa na kigugumizi.

Amesema Bunge limeshindwa kumhudumia na kumlipia matibabu kama ambavyo inapaswa kuwa lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa Bunge ambaye amethubutu hata kwenda kumuona. 

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.