Kuleta ndugu wa nne ili kuongezewa damu kwa tajwa kuwa kikwazo, mkoani Katavi
MPANDA
Baadhi ya Wananchi mkoani Katavi wamekitaja kitendo cha kutakiwa kuleta
ndugu wanne wa kujitolea damu pindi mgonjwa anapo kuwa na tatizo la kuishiwa
damu kuwa kikwazo katika huduma ya afya .
Wamesema hayo kwa nayakati tofauti wakati wakizungumza na Mpanda radio fm
na kueleza kuwa hali hiyo ndiyo inayo chochea vitendo vya rushwa ili kupata
huduma.
Kwa uapande wake mratibu wa damu salama wa
hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Khadija
Juma amesema kwa mwezi hutumika chupa 350 na inaingiza chupa 400
mpaka 600 hivyo kiwango hicho kinakidhi mahitaji ya wagonjwa.
Aidha amewaomba kujenga tabia ya kujitolea damu kwa kwa
hiari,wakati wote na siku yoyote katika masaa ya kazi.
Wiki iliyopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, akiwa kwenye
uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
amezitaka Hospitali na vituo vya Afya nchini kuhakikisha wagonjwa hawauziwi
damu.
Source Neema
Manyama
Editor Alinanuswe Edward
Source Neema Manyama


Comments
Post a Comment