George Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia, huku akiahidi kutimiza matarajio ya wananchi



George Weah ameapishwa kuwa rais  wa Liberia, huku akiahidi kutimiza matarajio ya wananchi.

Nyota huyo wa zamani wa kandanda duniani George Opong Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.

Weah amechukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.

Kuingia kwa Weah madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu mwaka 1944.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.