Chama cha walimu CWT mkoa wa Katavi cha mpa tano JPM

Chama cha Walimu CWT  mkoa wa Katavi kimempongeza rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kutangaza kutoa fedha bilioni 200 ili zilipe madeni ya ndani yakiwemo ya walimu.

Akizungumza na Mpanda radio fm kwa njia ya simu katibu wa chama cha CWT mkoa wa Katavi mwalimu Hamiss Chinahova amesema hatua ya serikali kulipa madeni hayo italeta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.

Katika hatua nyingine amewataka waalimu kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa weledi zaidi ili ilete tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.


Mwaka 2017 walimu nchini Tanzania walitishia kugoma kwa kile walicho kitaja kuwa ni kukithiri kwa madai dhidi ya serikali wakisema inawavunja morari ya kazi.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.