CHADEMA YASEMA RUSHWA NDIO CHANZO KWA VIGOGO WAKE KUHAMIA CCM



DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Chama  Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji amesema kuendelea kuhama kwa  Madiwani na baadhi ya wanachama wa chama hicho chanzo chake ni rushwa na sio sababu nyingine kama wao wanavyotoa.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vincent Mashinji leo kufuatia  kujiuzulu kwa madiwani wawili wa  CHADEMA Mkoani  Iringa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi   (CCM).

Aidha katibu huyo wa CHADEMA ameendelea kwa kusema sio tu madiwani ambao wanafatwa na kupewa rushwa bali hata kuna wabunge na viongozi wa juu kabisa ambao wanafatwa na kushawishiwa kwa kupewa rushwa.


Mpaka sasa Manispaa ya Iringa Mjini imepoteza madiwani wa Kata sita ambao wote baada ya kujiuzulu wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.