CCM YASHINDA KWA KISINDO SINGIDA


SINGIDA:

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimepata ushindi wa kishindo katika majimbo ya Singida Kaskazini Mkoani Singida.
Wagombea wa chama hicho Justine Monko Joseph wa Singida Kaskazini katangazwa leo kuwa mshindi kwa kura zaidi ya 20,000 kati ya 22,000 zilizopigwa.
Kwa upande wa Songea Mjini, mgombea wa CCM, Damas Ndumbaro amepata ushindi kwa kura 45,162 na kumuacha mgombea wa CUF aliyepata kura 608.
Katika Jimbo la Longido, umefanyika kwa amani na utulivu mkubwa huku baadhi ya watu wakimiminika katika vituo vya kupiga kura kutimiza demokrasia yao ya kumchagua mbunge wa jimbo hilo.
Uchaguzi huo unarudiwa kufanyika baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ubunge wa Mbunge wa Chadema, Onesmo ole Nangole kutokana na ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi katika ushindi wake.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.