Botswana imemshutumu Rais wa Marekani kwa kusema mataifa ya Afrika ni machafu



GABORONE:

Serikali ya Botswana imemshutumu Rais wa Marekani kwa kusema mataifa ya Afrika ni machafu na kusema tamko lake rais huyo ni la kukosa kuwajibika, la kukera na ubaguzi wa rangi.

Bw Trump amesema hayo alipokuwa akizungumzia sera ya uhamiaji ya Marekani, ambapo ameeleza kuwa watu kutoka Haiti, El Salvador na nchi za Afrika hawafai kuruhusiwa kuingia kama wahamiaji Marekani.

Botswana imesema kupitia taarifa kwamba imemwita balozi wa Marekani nchini humo kufafanua iwapo Marekani inachukulia taifa hilo la kusini mwa Afrika kama taifa chafu  na taifa la mabwege.

Taarifa hiyo ya Botswana imesema tamko la Trump ni la kukosea heshima taifa ambalo lina urafiki wa kufana na uhusiano wa kibalozi.


Botswana imeitaka jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika Sadc pamoja na Umoja wa Afrika kushutumu tamko hilo la Trump.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.