Benki Kuu ya Tanzania(BoT) ya zifuta benki tano na kuziweka chini ya sheria ya ufirisi


DAR ES SALAAM.

 Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia  leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited.

BoT imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)( cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi.

Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.