Azika watoto wake wawili wakiwa hai kwa tuhuma ya wizi wa mahindi


Mtu mmoja nchini Burundi aliyefahamika kwa jina la Nyandwi Elias wa eneo la Bubanza, anatafutwa na Polisi kwa kosa la kuwapiga na kuwafukia ardhini watoto wawili, akiwatuhumu kuiba mahindi shambani kwake.
Tukio hilo limetokea January 14, 2018 baada ya majirani kusikia kelele za watoto wakilia, na ndipo walipenda na kukuta watoto hao waliojulikana kwa jina la Egide Bigirimana na Tuyisenge wenye umri wa miaka 10 na 12,  wakiwa wamefukiwa na kuachwa sehemu ya kichwa.
Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za watoto Jacques Nshimirimana, (FENADEB)  amesema kitendo hiko cha ukatili kinadhihirisha ni kwa namna gani watu wa Burundi hawana uelewa wa haki za watoto, kwani vitendo kama hivyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara, ambapo watoto wawili walikatwa mikono baada ya kukutwa wakiiba mahindi.
Jeshi la Polisi limesema linaendelea kumtafuta mthuhumiwa huyo ili achukuliwe hatua za kisheria, na kutoa somo kwa wengine.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.