AHUKUMIWA KWA KUMTUKANA MKUU WA WILAYA /TABORA


TABORA:
Mahakama  ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imemhukumu mkazi wa mtaa wa barabara ya Mbutu, Mohamed Ahmed (54) kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumtishia na kumtolea lugha ya matusi Mkuu wa Wiilaya hiyo, John Mwaipopo. 

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Elimajidi Kweyamba, alidai mahakamani hapo kwamba mshitakiwa, alitenda kosa hilo Januari 09, mwaka huu, saa 1:05 usiku katika maeneo ya barabara kuu ya lami ya Igunga mjini. 

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi, Kweyamba amesema kuwa mshitakiwa huyo alimtolea Lugha ya matusi Kiongozi huyo wa Wilaya wakati akitekeleza majukumu ya agizo la upandaji miti kama lilivyotolewa maelekezo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani. 

Aidha, mwendesha mashtaka amedai kwamba katika kosa la pili, muda huo huo na tarehe hiyo hiyo, mshitakiwa akiwa na nia ovu, alimtishia maisha kwa maneno Mkuu wa Wilaya kuwa atamwonyesha na atahakikisha anahama Igunga kwa kumfanyia kitu kibaya. 

Kabla ya kutoa hukumu, Hakimu Milanzi amesema kwa kuwa mshtakiwa amekiri mwenyewe makosa, atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitatu gerezani, mwaka mmoja kwa kosa la kwanza na miwili kwa kosa la pili.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.