34 wafariki kwa ajali ya basi

Afisa Mkuu wa idara ya polisi wa trafiki maeneo ya Bonde la Ufa, Zero Arome amesema ajali hiyo imetokea kwenye barabara kuu ya kutoka Nakuru kuelekea Eldoret Magharibi mwa Kenya.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limeandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter, kuhusiana na ajali hiyo ambapo mabaki ya magari hayo yaliyohusika kwenye ajali yalisalia katika eneo la tukio, huku majeruhi wakipelekwa katika Hospitali za Nakuru Level Five na ile ya Molo Sub-County.

Comments
Post a Comment