Viongozi na Wanachama wa chama cha mapinduzi ccm mkoani Tabora wameipongeza halmashauri kuu ya ccm Taifa kwa kukubali kuwapokea wanachama wapya waliojiunga na chama hicho hivi karibuni.
Na Mussa Mbeho,Tabora.
Viongozi na Wanachama wa chama cha mapinduzi ccm mkoani Tabora wameipongeza halmashauri kuu ya ccm Taifa kwa kukubali kuwapokea wanachama wapya waliojiunga na chama hicho hivi karibuni.
Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya viongozi na wanancham wa ccm mkoani humo wakati wakizungumza na Mpandaradio fm mara baada ya kikao cha halmashauri kuu ya ccm Taifa kuwapokea wananchama wapya mapema hii leo Ikulu jijini Dareesalaam.
Athumani Mtunda na Mwamba Zuberi ni baadhi tu ya wananchama wa chama cha mapinduzi ccm mkoani humo wamesema wamefurahahi kuona viongozi hao wakirudi ccm kwa kuwa chama cha mapinduzi ndio chama pekee chenye kuwaletea maendeleo watanzania.
Aidha wananchama hao wamewashauri viongozi wote wa vyama vya upinzani ambao bado hawajajiunga na chama cha mapinduzi ccm wajiunge na chama hicho ili waweze kuchapa kazi kwa maendeleo ya Taifa.
Nae katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Tabora mjini Bi Vaileth Lukas kasanga amesema kuwa chama cha mapinduzi ccm ni mzazi wa vyama vingine hivyo anawapongeza viongozi hao kwa kurejea ndani ya cham hicho huku akiwashauri kuwa na msimamo juu ya maamuzi yao .
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Sikonge bwana Emanuel Alex amesema anawapongeza wananchama hao wapya kwa kujiunga na ccm huku akiwaomba wawe watulivu na kuchapa kazi kwa kumsaidia Rais Daktari John pombe joseph magufuri ili Tanzania iweze kusonga mbele kimaendeleo.

Comments
Post a Comment