TCRA NA POLIS WAZUNGUMZIA ACCOUNT YA MANGE KIMAMBI



Jeshi la Polisi limetaka liachwe liendelee kufanya kazi yake kwa weledi katika kushughulikia suala la Mtanzania aishiye ughaibuni, Mange Kimambi, ambaye anatuhumiwa kuchapisha taarifa zinazodaiwa kuwatusi mitandaoni watu mbalimbali wakiwamo viongozi.

 Akizungumza na Nipashe  kuhusiana na uwezekano wa wao kuifunga akaunti ya Kimambi ikiwa sehemu ya hatua wanazochukua kwa sasa, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, alisema ni kweli jeshi lao linalifanyia kazi suala hilo.
Hata hivyo Mwakalukwa hakutaka kukubali au kukataa juu ya kile kilichodaiwa kutokea kwenye akaunti ya Kikambi na badala yake kutaka apewe muda wa kulifanyia kazi ndipo alitolee maelezo ya kina.
Hili jambo lina mambo mengi sana. Watu wengi wanahusika na taasisi nyingi (pia) zitahusika kulishughulikia, Hivyo tunaendelea kupokea mawazo ya watu mbalimbali kuhusu namna ya kwenda nalo… mawazo wanayotupa tunayafanyia kazi lakini naomba mtuache kwanza tunaendelea kulishughulikia,” alisema Mwakalukwa.
Aidha wakati Msemaji wa Polisi akisema hayo, TCRA ilisema kuwa haiwezi kufunga wala kuingilia akaunti ya Kimambi kwa sababu huo siyo wajibu wake kisheria.
Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala, aliiambia Nipashe kuwa mamlaka yao haina nguvu za kisheria kufanya kazi hiyo bali wenye wajibu wa kufanya hivyo ni kitengo cha kudhibiti uhalifu wa mitandaoni cha Jeshi la Polisi.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.