Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake miaka 40 iliyopita.
MPANDA
Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na
halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa
kwake miaka 40 iliyopita.
Hayo yamebainishwa na wakazi wa Kata ya Katumba
wanaotumia soko hilo ambapo wamesema wanaishi kwa taharuki ya kukumbwa na
kipindupindu kutokana na kukithiri kwa uchafu na ukosefu wa choo katika soko
hilo.
INSERT…. WAKAZI KATUMBA
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya kibiashara
wamesema wanatozwa kuanzia shilingi elfu sita na mia tano huku wafanyabishara
wanaouzia bidhaa chini wakilipa ushuru kila wanapouza lakini hawaoni jitihada
zozote zikifanywa na mamlaka.
Kwa upande wao mwenyekiti wa soko hilo Bw.Leonard
Kigwasu na Afisa Mtendaji wa vijiji vya Mnyaki A na B Bw.Kombo Masatu wamekiri
kuwepo kwa uchafu sokoni hapo huku akisema choo kinatarajiwa kukamilika katika
kipindi cha miezi miwili ijayo.
Source Isack Gerald
Editor Alinanuswe Edward
Comments
Post a Comment