Rais wa zamani wa Yemen Abdullah Saleh 'auawa'


Aliyekuwa rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh ameuawa katika mapigano na washirika wake wa zamani, taarifa zinasema.

Mashirika ya habari yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi yamewanukuu maafisa wakitangaza mwisho wa mzozo wa wanamgambo wahaini na kiongozi wao.

Duru katika chama chake Bw Saleh cha General People's Congress pia wamethibitisha kwamba amefariki, kwa mujibu wa Al Arabiya TV.

Picha na video zilizosambazwa mtandaoni zimeuonesha mwili wa mwanamume anayefanana na Bw Saleh ukiwa na kidonda kichwani.


Hadi kufikia wiki iliyopita, wafuasi wa Bw Saleh walikuwa wanapigana pamoja na wapiganaji wa jamii ya Houthi dhidi ya rais wa sasa wa Yemen Abdrabbuh Mansour Hadi.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.