RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AVUNJA REKODI KATIKA AWAMU ZOTE KWA MSAMAHA WA WAFUNGWA WALIO HUKUMIWA KUNYONGWA
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.
Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake.
Miongoni mwa walio achiwa huru ni mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha ambao walifungwa tangu 2004
Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao.
Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha
Maadhimisho ya mwaka huu kauli mbiu yake ni ‘Uhuru Wetu
ni Tunu, tuudumishe, Tulinde raslimali zetu, tuwe wazalendo, Tukemee rushwa na
Uzembe, yanafanyika mjini hapa.’

Comments
Post a Comment