PAPA ATAKA SALA YA USITUTIE KATIKA VISHAWISHI
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba maombi maarufu ya Kikristo ya Baba Yetu yafanyiwe marekebisho.
Anataka sehemu ambayo huzungumzia vishawishi ilitafsiriwa vibaya.
Asema tafsiri kwamba "Usitutie katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" iangaziwe upya akisema tafsiri iliyofanywa si sahihi kwa sababu Mungu huwa hawaongozi binadamu kutenda dhambi.
Papa amependekeza watu watumie "usituache tukaingia katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" badala yake.
Alitoa pendekezo hilo akizungumza katika runinga ya Italia Jumatano usiku.
Ombi la Baba Yetu ndilo linalofahamika vyema zaidi miongoni mwa maombi ya Kikristo.
Papa Francis amesema Kanisa Katoliki nchini Ufaransa sasa linatumia tafsiri hiyo ya "usituache tukaingia katika vishawishi" kama mbadala, na kwamba jambo kama hilo linafaa kufanywa kote duniani.
"Usiniache nikaingia kwenye vishawishi kwa sababu ni mimi nitakayeanguka, si Mungu anayetutia katika vishawishi na kisha kutazama nilivyoanguka," aliambia runinga ya TV2000, runinga ya kanisa Katoliki Italia.
"Baba hawezi kufanya hivyo, baba hukusaidia huinuke upesi."

Comments
Post a Comment