MWENYEKITI WA KIJIJI CHA STALIKE MKOANI KATAVI AGOMA KUACHIA NGAZI


MPANDA/KATAVI

Mwenyekiti wa Kijiji cha Stalike Bwana Christopher Mrisho amesema hayuko tayari kuachia ngazi kwa tuhuma za kuwachangangisha pesa wananchi kinyume na sheria

Bwana Mrisho ameiambia Mpanda Radio kuwa haoni umuhimu wa kufanya hivyo kwani ni wananchi wenyewe ndio waliomba kuchangisha pesa hizo

Imedaiwa kuwa Bwana Mrisho  amewachangisha wananchi hao kwa awamu mbili tofauti zaidi ya sh milioni moja kwa madai kuwa anaenda kuonana na waziri mkuu wa Tanzania ili kuwasaidia kutatua mgogoro kati ya wananchi hao na mamlaka ya hifadhi za misitu Tanzania


Mwenyekiti huyo anadaiwa kuwachangisa baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao waliondolewa na serikali katika makazi hayo ikidaiwa kuwa walivamia hifadhi ya msitu

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.